Mwanafalsafa Arthur Schopenhauer alisema maisha yetu ni kama mto ambao unatiririka kwenye kingo mbili.
Ukingo wa kwanza ni msongo (stress), hapa ni pale ambapo unakuwa na mambo mengi ya kufanya kuliko muda au uwezo wako wa kuyafanya.
Ukingo wa pili ni uchoshi (boredom), ambapo unakuwa na muda mwingi ambao huna kitu cha kufanya.
Watu wengi wamekuwa wanaendesha maisha yako kwenye moja ya kingo hizi.
Wapo ambao wanaendesha maisha yao kwenye ukingo wa msongo, kila wakati wapo na vitu vingi vya kufanya kuliko muda na uwezo wao. Maisha ya aina hii yanachosha na kuleta madhara kwenye afya na maisha kwa ujumla.
Na wapo ambao wanaendesha maisha yao kwenye ukingo wa uchoshi, wanakuwa na muda mwingi ambao hawana cha kufanya. Hivyo hawa hujikuta wakijiingiza kwenye mambo yasiyo sahihi na kutengeneza matatizo zaidi kwenye maisha yao.
Kama ilivyo kwa mto, unatiririka katikati ya kingo hizo na siyo kwenye ukingo mmoja, hivyo pia ndivyo unavyopaswa kuyaendesha maisha yako, kwa kuwa katikati ya msongo na uchoshi. Pangilia vizuri muda wako, usizidishe unayopanga kufanya na wala usiwe na muda mwingi ambao huna cha kufanya.
Ukiweza kutawala vizuri muda wako na yale unayofanya, utaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante sana Makirita Aman nimejifunza kitu kikubwa sana hapa
LikeLike
Vizuri Hendry,
Fanyia kazi kile ulichojifunza.
LikeLike