“Don’t tell yourself anything more than what the initial impressions report. It’s been reported to you that someone is speaking badly about you. This is the report—the report wasn’t that you’ve been harmed. I see that my son is sick—but not that his life is at risk. So always stay within your first impressions, and don’t add to them in your head—this way nothing can happen to you.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.49
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo,
Ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari ONA VITU KAMA VILIVYO…
Vitu huwa vinatokea kwenye maisha yetu, halafu sisi tunavipa maana,
Kinachotuumiza kwenye maisha siyo vitu ambavyo vimetokea, bali maana tunayojipa kwenye vitu ambavyo vimetokea.
Hizi maana ndiyo zinazotusumbua sana.
Hivyo kama hutaki kusumbuka, kama hutaji kujiumiza, basi acha kuvipa vitu maana isiyokuwepo.
Vione vitu kama vilivyo bila ya kuongeza maana yoyote ile.
Umeambiwa mtu anakusema vipaya, hiyo ni taarifa tu umepewa, hujamkuta akikusema vibaya na hata kama amekusema vibaya hakuna chochote ambacho maneno yake yameleta kwenye maisha yako.
Umemsalimia mtu hakuitika haimaanishi kwamba ameacha kuitika makusudi au amekununia au ana visa na wewe, ni kwamba hajaitika.
Umejaribu kitu ukashindwa, haimaanishi kwamba wewe huwezi chochote au kila mara umekuwa unashindwa au una bahati mbaya.
Tumekuwa tunatengeneza hadithi ambazo zinatuumiza kuliko matukio ambayo yamezalisha hadithi hizo.
Hivyo kama unataka kuwa na maisha tulivu, ona vitu kama vilivyo na acha kabisa kujitengenezea maana au hadithi ya kile kinachotokea.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuona vitu kama vilivyo na kuacha kujitengenezea maana zinazokuumiza.
#OnaVituKamaVilivyo #AchaKutengenezaMaanaIsiyokuwepo #MamboUsiyitarajiaHutokea
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1