“When the problem arose for us whether habit or theory was better for getting virtue—if by theory is meant what teaches us correct conduct, and by habit we mean being accustomed to act according to this theory—Musonius thought habit to be more effective.”
—MUSONIUS RUFUS, LECTURES, 5.17.31–32, 5.19.1–2
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari HAKUNA MUDA WA NADHARIA, LETA MATOKEO…
Kuweka malengo na mipango ni kuzuri sana,
Kupitia mikakati mbalimbali na hatua za kuchukua ni jambo jema.
Lakini yote hayo hayana maana kama hakuna matokeo.
Matokeo ndiyo kitu unachoweza kukipima, kitu kinachokuwezesha kutoka hapo ulipo sasa na kupiga hatua.
Nadharia, hasa kwenye kupanga na kufuatilia yale uliyopanga, lakini hatua zinatokana na matokeo uliyozalisha.
Hivyo weka muda na nguvu zaidi kwenye kuchukua hatua ili kuzalisha matokeo ambayo yanaonekana na kupimika.
Kwa kila unachopanga, anza kuchukua hatua hapo hapo baada ya kupanga, usiendelee kusubiri.
Umesema kuna mtu utawasiliana naye, chukua simu na wasiliana naye hapo hapo.
Umepanga kuna hatua utachukua, anza mara moja kuchukua hatua hizo wakati huo huo.
Kuwa mtu wa KUCHUKUA HATUA SASA, kwa sababu matokeo yana nguvu kuliko nadharia.
Na usiogope kwamba hujui au hujawa tayari na hivyo utashindwa, kushindwa ni sehemu ya kujifunza.
Kushindwa ni sehemu ya matokeo, ambayonina nguvu kuliko nadharia za kujua na kupanga pekee.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuweka nguvu kubwa kwenye kuchukua hatua na kuzalisha matokeo. Leo nenda kajiambia NITACHUKUA HATUA SASA, kwa kila unachopanga kufanya, na utaona jinsi siku yako itakuwa ya tofauti sana.
#ZalishaMatokeo #ChukuwHatuaSasa #UsiweMtuWaNadhariaPekee
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1