“You’ve endured countless troubles—all from not letting your ruling reason do the work it was made for—enough already!”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 9.26

Ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari HATUA YA KUCHUKUA KUMALIZA MATATIZO YAKO…
Hatua ya kuchukua ili kumaliza matatizo yako ni kutumia vizuri akili yako na kufikiri kwa kina.
Matatizo na changamoto nyingi tunazopitia kwenye maisha ni kwa sababu tunachukua hatua bila ya kufikiri.
Tunasukumwa na hisia kufanya vitu fulani,
Au tunaona wengine wakifanya na sisi tunafanya.

Ukitumia akili yako kwa usahihi, ukafikiri kwa kina kwa kila unachofanya, utaona hatua sahihi za kuchukua, ambazo ni kinyume kabisa na hatua unazokuwa unachukua kwa hisia au kufuata mkumbo.
Kinachotutofautisha sisi binadamu na wanyama wengine ni uwezo wetu wa kufikiri.
Lakini utashangaa wengi wanaendesha maisha yao bila kufikiri kabisa, wanaendeshwa na hisia au kuangalia wengine wanafanya nini na wao wanafanya.

Kama unataka kuwa na maisha bora, kama unataka kupiga hatua zaidi, kama unataka kutoka pale ulipokwama sasa, njia ni moja, tumia akili yako na fikiri kwa kina na usahihi.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia akili yako na kufikiri kwa kina na usahihi ili kuondokana na matatizo mbalimbali.
#TumiaAkiliYako #FikiriKwaUsahihi #UsiendeshweNaHisia #UsifuateKundi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1