“For nothing outside my reasoned choice can hinder or harm it—my reasoned choice alone can do this to itself. If we would lean this way whenever we fail, and would blame only ourselves and remember that nothing but opinion is the cause of a troubled mind and uneasiness, then by God, I swear we would be making progress.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.19.2–3

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo,
Ni siku mpya na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KABLA HUJALAUMU WENGINE, TAMBUA MCHANGO WAKO MWENYEWE…
Huwa tunaendesha maisha yetu kwa kulalamikia na kulaumu wengine, lakini kwa hakika hakuna mtu yeyote anayestahili lawama zetu ila sisi wenyewe.
Pale ambapo mambo ambayo hatukutegemea yatokee yanatokea kwetu, tumekuwa tunakimbilia kutafuta nani au nini kimesababisha ili tupeleke lawama zetu kwenye watu au vitu hivyo.
Lakini hili siyo sahihi na wala halina msaada wowote kwako.

Chochote unachopitia au kukutana nacho kwenye maisha, kimeanza na wewe mwenyewe, umekisababisha wewe mwenyewe.
Hata kama kuna wengine wameshiriki kukifanya, wewe ndiye uliyeruhusu hilo litokee.
Hivyo kabla hujamlaumu au kumlalamikia yeyote, jiulize kwanza wewe mwenyewe umeruhusuje kitu kama hicho kutokea.

Kama ni mtu amekuibia, kukulaghai au kukutapeli, kabla hujamlaumu mtu huyo jua kabisa wewe ndiyo umempa nafasi ya yeye kufanya hivyo. Ni wewe mwenyewe uliyemwamini ah uliyekosa umakini wa kutosha, mpaka kuruhusu hali kama hiyo kutokea.
Ukiacha kulaumu wengine na kuangalia mchango wako katika usababishi, utaweza kuzuia changamoto nyingi unazokutana nazo zisijirudie tena.

Jijengee tabia hii ya kutambua mchango wako kwenyewe kwenye kila hali unayojikuta na utaweza kujua hatua sahihi kwako kuchukua ili kuondokana na changamoto mbalimbali.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuacha kulaumu wengine na kuangalia mchango wako mwenyewe kwenye kila hali unayopitia.
#UsilaumuWengine #WeweNdiyeMhusikaMkuu #LawamaHazijengi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1