“It is said that if you would have peace of mind, busy yourself with little. But wouldn’t a better saying be do what you must and as required of a rational being created for public life? For this brings not only the peace of mind of doing few things, but the greater peace of doing them well. Since the vast majority of our words and actions are unnecessary, corralling them will create an abundance of leisure and tranquility. As a result, we shouldn’t forget at each moment to ask, is this one of the unnecessary things? But we must corral not only unnecessary actions but unnecessary thoughts, too, so needless acts don’t tag along after them.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 4.24

Shukrani ndiyo namna pekee ya kuianza siku hii nyingine nzuri tuliyoiona leo,
Tumeiona siku hii siyo kwa nguvu zetu, akili zetu au kwa sababu tunastahili sana,
Bali tumeiona siku hii kwa sababu kazi yetu bado haijaisha hapa duniani, hivyo tukaitumie vyema siku hii kwa kufanya kazi zetu kwa usahihi.
Njia pekee ya kushukuru kwa siku hii tuliyonayo siyo kwa maneno, bali kwa matendo.
Na matendo hayo ni kuishi kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na kuongozwa kwa mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA, kwa kuishi hivyo leo, utaweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Asubuhi ya leo tutafakari FANYA MACHACHE, KWA UBORA ZAIDI…
Rafiki, kilio cha kila mtu zama hizi ni kwamba hakuna muda kabisa,
Mambo ya kufanya ni mengi, lakini muda wa kuyafanya ni mchache.
Hivyo wengi wanakuwa wamekwama kwenye maisha yao, wakitamani kupata muda zaidi lakini hilo halitokei.

Menta wangu Seneca analikataa hilo, hakubali kwamba huna muda, anasema wazi kwamba tatizo la muda siyo kwamba hatuna wa kutosha, ila tunao mwingi sana mpaka tunachagua kuupoteza. Kwenye kitabu cha Seneca kinachoitwa ON THE SHORTNESS OF LIFE, ametuonesha wazi jinsi tunavyoyapoteza maisha yetu na hatua sahihi za kuchukua.

Na mimi pia nakukatalia kwenye hilo la muda, nakuambia siyo kwamba una tatizo la muda, bali una tatizo la vipaumbele. Kwenye kitabu changu kinachoitwa PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, nimekuonesha jinsi unavyoweka vipaumbele vyako vizuri na ukaokoa masaa mawili kwenye kila siku yako, hata kama upo bize kiasi gani.

Leo rafiki, nina zoezi ambalo nataka nikushirikishe, zoezi la kujaribu kwa wiki nzima, kisha kupima matokeo yake mwishoni.
Tunaona tatizo la muda ni kuwa tunaupoteza kwa kukosa vipaumbele.
Sasa kwa juma hili moja, nataka ukapunguze kabisa yale unayofanya, ufanye machache sana, lakini kwa ubora wa hali ya juu.

Utatumia mwongozo wetu wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA katika kuweka vipaumbele vyako.
Kabla hujafanya chochote, jipe sekunde 30 na jiulize maswali haya;
1. Je kwa kufanya kitu hiki kunaifanya afya yangu kuwa bora kuliko ilivyo sasa?
2. Je kwa kufanya kitu hiki, kuna fedha ambayo naingiza kwenye mfuko wangu?
3. Je kwa kufanya kitu hiki nitakuwa na hekima zaidi ya niliyonayo sasa?
Kama jibu ni ndiyo kwenye swali lolote hapo juu basi fanya.
Lakini kama majibu ni hapana kwenye maswali yote, acha kufanya kitu hicho mara moja.
Yaani acha tu kufanya, usijiambie lakini… au kuanza kutafuta sababu za kuunga unga.
Kama kitu hakiboreshi afya yako, hakikuingizii fedha na hakikupi hekima, hupaswi kukifanya. Ni hivyo tu.

Jaribu zoezi hili kwa wiki moja, kisha nitumie matokeo ambayo utakuwa umeyapata. Nakuhakikishia, kwa wiki moja utakayofanya hilo, utakuwa na muda mwingi mpaka utajishangaa.

( MUHIMU Ukijipatia nakala tete ya kitabu cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA, nitakutumia bure kitabu cha Seneca cha ON THE SHORTNESS OF LIFE pamoja na uchambuzi wake. Tuma tsh elfu 5 ya kitabu pamoja na email yako na utatumiwa kitabu pamoja na zawadi. Ni kwa leo tu)

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuweka vipaumbele vyako kwa usahihi, kwa kutumia mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA. Usifanye chochote ambacho hakiboreshe afya yako, hakikuingizii fedha na hakikufanyi uwe na hekima zaidi.
#MudaUnaoWaKutosha #WekaVipaumbeleSahihiKwako #AfyaUtajiriHekima

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1