“Consider who you are. Above all, a human being, carrying no greater power than your own reasoned choice, which oversees all other things, and is free from any other master.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.10.1
Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi hii nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NGUVU ILIYOJIFICHA NDANI YAKO…
Haijalishi unapitia hali gani,
Haijalishi ni magumu kiasi gani unayopitia,
Haijalishi ni maumivu kiasi gani unayokutana nayo,
Haijalishi kwa nje unaonekana dhaifu kiasi gani,
Wewe una nguvu kubwa sana iliyojificha ndani yako.
Hii ni nguvu ambayo hakuna mwenye uwezo wa kuizuia au kuichukua.
Hii ni nguvu inayokufanya wewe kuwa mtu, inayokupa wewe uhuru wowote unaotaka.
Nguvu hiyo ni uwezo wa kutoa maana kwenye yale yanayotokea.
Ni wewe pekee ambaye una nguvu ya kuamua kile kinachotokea kina maana gani kwako.
Wengine wanaweza kufanya kitu ili kukuumiza, lakini wewe una nguvu ya kukichukulia kama sehemu ya kukomaza imani yako.
Wengine wanaweza kufanya kitu ili kukurudisha nyuma, lakini wewe kikawa sehemu ya kupima uwezo wako mkubwa.
Ile maana unayoweka kwenye yale yanayotokea na unayokutana nayo, ina mchango mkubwa sana kwenye matokeo unayopata na ubora wa maisha yako.
Chagua leo kutumia nguvu hiyo kubwa iliyojificha ndani yako, nguvu ya kutengeneza maana nzuri kwako kwenye kila baya na gumu unalopitia.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutengeneza maana nzuri kwa chochote unachopitia ili kuendelea kujiimarisha zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1