“What if someone despises me? Let them see to it. But I will see to it that I won’t be found doing or saying anything contemptible. What if someone hates me? Let them see to that. But I will see to it that I’m kind and good-natured to all, and prepared to show even the hater where they went wrong. Not in a critical way, or to show off my patience, but genuinely and usefully.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 11.13
Ni nani awezaye kusema kwa nguvu zake na ujanja wake ameweza kuiona siku hii mpya ya leo?
Kwa hakika ni mpumbavu pekee.
Wenye hekima wanajua ni bahati kuiona siku nyingine mpya kama ya leo.
Hivyo wanaitumia vizuri kila siku wanayoipata, kwa sababu wanajua inaweza kuwa ndiyo siku ya mwisho kwao kuwa hapa duniani.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JINSI YA KUWAKABILI WANAOKUDHARAU NA WANAOKUCHUKIA…
Vipi kama mtu amechagua kukudharau kutokana na maisha yako au kile unachofanya?
Mwache akudharau, wajibu wako ni kuhakikisha hufanyi kitu chochote cha kujidharaulisha.
Vipi kaka mtu amechagua kukuchukia kutokana na maisha yako au kile unachofanya?
Mwache akuchukie, wajibu wako ni kuhakikisha huna chuki na mtu yeyote.
Dharau na chuki vinaeleza zaidi hali ya mtu anayevifanya kuliko yule anayefanyiwa.
Hii ina maana kwamba, kama mtu anakudharau, basi jua anajidharau zaidi yeye kuliko anavyokudharau wewe.
Kama mtu anakuchukia basi jua anajichukia zaidi yeye kuliko anavyokuchukia wewe.
Huwezi kuwapangia wengine wakuchukulieje au wawe na hisia gani juu yako.
Bali unaweza kuchagua misingi ambayo utaiishi kwenye maisha yako, ambayo yanakufanya uwe na maisha bora kwa upande wako.
Wengine wanakuchukuliaje hiyo siyo biashara yako, na usiruhusu hilo likusumbue.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kwenda kukabiliana na wenye dharau na chuki kwa kuchagua kuyaishi maisha yako na kuwaacha waishi maisha waliyochagua pia.
#UsitakeKumfurahishaKilaMtu #IshiKwaMisingiYako #JaliMamboYako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1