“When forced, as it seems, by circumstances into utter confusion, get a hold of yourself quickly. Don’t be locked out of the rhythm any longer than necessary. You’ll be able to keep the beat if you are constantly returning to it.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.11
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii mpya tuliyoiona leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari DUMISHA UTULIVU, DUMISHA UDHIBITI…
Kama ambavyo tunajua, pamoja na maandalizi makubwa ambayo tunakuwa nayo, bado kuna mambo yatakayotokea, ambayo hatukutegemea yatokee.
Na huo ndiyo wakati muhimu sana wa kupima ukomavu wa mtu.
Kwa sababu wale ambao hawajakomaa, hupata taharuki na kuona kama ndiyo mwisho wa kila kitu.
Huona dunia haina usawa na kila kibaya kinatokea kwao.
Lakini kwa wale wenye ukomavu, kinapotokea kile wasichotegemea, huwa ndiyo wakati mzuri kwao kujifunza, kwamba mambo huwa yanayokea, kwa namna yao yenyewe na siyo kwa mapenzi yetu sisi.
Katika wakati huu, huwa wanadumisha utulivu na udhibiti wao, hawaruhusu chochote kinachotokea nje kiwavuruge ndani yao.
Wanaweza kushtuka kwa kile kikichotokea, lakini mara moja wanarudi kwenye utulivu na udhibiti wao. Hawatumii muda mwingi kwenye kuangalia nini kimetokea na kwa nini kimetokea. Wanatumia muda mwingi kwenye hatua sahihi kwao kuchukua ili kuendelea kuwa na utulivu ma udhibiti.
Ukishapoteza utulivu na udhibiti wako, unakuwa kwenye hatari ya kufanya maamuzi mabovu na yatakayokugharimu.
Ndiyo maana wale wanaotaka kukuvuruga au kukutapeli, huwa wanaharibu kwanza utulivu na udhibiti wako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku na kudumisha utulivu na udhibiti bila ya kujali ni nini kimetokea au kinaendelea kwenye maisha yako.
#UtulivuNiMuhimu #UsipotezeUdhibitiWako #UsiyotegemeaYatatokea
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1