“The best way to avenge yourself is to not be like that.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.6
“How much better to heal than seek revenge from injury. Vengeance wastes a lot of time and exposes you to many more injuries than the first that sparked it. Anger always outlasts hurt. Best to take the opposite course. Would anyone think it normal to return a kick to a mule or a bite to a dog?”
—SENECA, ON ANGER, 3.27.2
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NJIA BORA YA KULIPA KISASI…
Kuna wakati watu wanatufanyia mambo ambayo yanayukasirisha sana, na tunaona hatuwezi kuwaacha hivi hivi, lazima tulipe kisasi.
Lakini kisasi chochote utakacholipa, hakitaondoa maumivu, badala yake kitayazidisha zaidi maumivu.
Hivyp njia bora kabisa kwako ya kulipa kisasi ni kutokufanya kile ambacho mtu amekufanyia. Kukataa kuwa kama yeye, hili linakupa wewe nguvu ma heshima.
Pata mfano huu, unapita njiani, ukakutana na mbwa na akakuuma, je utalipa kisasi kwa wewe kumuuma mbwa huyo?
Jibu ni hapana, hutajisumbua na mbwa huyo, kwa sababu unajua hata ukimuuma, haitakusaidia wewe chochote, zaidi ni kupata sumu kutoka kwake.
Hivyo ndivyo unavyopaswa kuwachukulia wale wote wanaokuudhi au kukufanyia mambo yanayoibua hasira ndani yako.
Kazana sana kujidhibiti usiwe kama wao.
Unapolipa kisasi, unakuwa umemdhihirishia mtu kwamba kile alichokifanya ni sahihi kabisa.
Mtu akikutukana na wewe ukamjibu kwa kumtukana, anapata uhalali kwamba ulistahili kabisa kutukanwa.
Lakini mtu akakutukana na wewe ukamjibu kwa kutokumtukana au kutokumjibu kabisa, inamfanya ajione yeye ni mjinga na mwenye matatizo.
Kataa kabisa kulipa ubaya wowote ambao mtu anakufanyia, hasa kwa makusudi na wewe utabaki kuwa juu yake.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutokulipa kisasi, siku ya kujidhibiti usilipe ubaya kwa ubaya.
#KisasiHakinaManufaa #UsilipeUbayaKwaUbaya #KupuuzaKunakupaNguvu
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1