“Some people with exceptional minds quickly grasp virtue, or produce it within themselves. But other dim and lazy types, hindered by bad habits, must have their rusty souls constantly scrubbed down. . . . The weaker sorts will be helped and lifted from their bad opinions if we put them in the care of philosophy’s principles.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 95.36–37

Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu,
Tumeiona siku hii nyingine, ambapo tuna nafasi ya kwenda kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari SAMBAZA HABARI NJEMA…
Unapojifunza kuhusu falsafa,
Unapojifunza kuhusu misingi sahihi ya kuyaendesha maisha yako,
Unapojifunza namna bora ya kukabiliana na changamoto pamoja na ugumu wa maisha unaokutana nao,
Una wajibu mkubwa sana wa kusambaza habari njema kwa wale ambao hazijawafikia.
Kwa sababu kujifunza tu wewe peke yako haitakuwa na msaada mkubwa kwa jamii, utakapoweza kuwashirikisha wengine wengi ndiyo itakuwa na msaada.
Hivyo kwa chochote kizuri unachojua na ukaona kuna wengine wanakabiliana na ugumu ambao unaweza kutatuliwa na kile unachojua, ni wajibu wako kuwashirikisha.

Sasa katika kuwashirikisha kuna wale ambao wakisikia kitu mara moja wanakielewa na kuchukua hatua.
Halafu kuna wale ambao ili wachukue hatua wanahitaji kusikia kitu mara nyingi mno.
Hivyo usikate tamaa pale unapowashirikisha watu kitu unachojua ni kizuri kwao halafu bado hawachukui hatua, jua unapaswa kuendelea kufanya hivyo bila ya kuchoka.

Na njia bora kabisa ya kuwashirikisha wengine habari hizo njema siyo kwa maneno, bali matendo, usieleze, onesha.
Watu wameshasikia sana maneno, wala hawayaamini tena.
Lakini matendo yana nguvu kubwa kuliko maneno,
Hivyo waoneshe ni jinsi gani wewe binafsi unakabiliana na changamoto kama zao au kuvuka ugumu ambao wao wanaupitia na hapo itakuwa rahisi kwao kuwa na hatua sahihi za kuchukua.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kusambaza habari njema ulizonazo wewe na zinazoweza kuwasaidia wengi e kupiga hatua zaidi. Shirikisha habari hizo njema kwa matendo na siyo maneno, onesha na siyo kuelezea.
#UnachojuaWafundisheWengine #UnapofundishaUnaelewaZaidi #OneshaUsieleze

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1