“You have proof in the extent of your wanderings that you never found the art of living anywhere—not in logic, nor in wealth, fame, or in any indulgence. Nowhere. Where is it then? In doing what human nature demands. How is a person to do this? By having principles be the source of desire and action. What principles? Those to do with good and evil, indeed in the belief that there is no good for a human being except what creates justice, self-control, courage and freedom, and nothing evil except what destroys these things.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.1.(5)
Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari VIASHIRIA VYA MAISHA MAZURI…
Nini maana ya maisha?
Kwa nini tunazaliwa?
Kwa nini tunakufa?
Maisha mazuri yakoje?
Haya ni baadhi ya maswali ambayo watu wamekuwa wanasumbuka nayo tangu enzi na enzi.
Maswali hayo ndiyo yamezalisha falsafa na dini mbalimbali, ambazo zote zimekuwa zinajaribu kujibu maswali hayo.
Kupitia Falsafa ya Ustoa tunajifunza kwamba maisha bora ni yale ambayo mtu anaishi kwa msingi fulani.
Kwamba, mali, utajiri, hadhi, mazingira na mengineyo hayaashirii maisha bora.
Bali misingi ambayo mtu anaiishi ndiyo inaashiria maisha bora.
Na msingi mzuri wa kuishi maisha mazuri ni ule ambao unazingatia HEKIMA, HAKI, KUJIDHIBITI, UJASIRI NA UHURU.
Nje ya msingi huo hakuna maisha mazuri.
Jijengee leo msingi utakaoufuata kwenye maisha yako, ili uwe na maisha bora wakati wote.
Ukawe na siku bora sana ya lei, siku ya kuishi kwa msingi sahihi ili kuwa ha maisha mazuri.
#MaishaBilaMsingiSiMaisha #MaishaMazuriYanaanzaNaWewe #MaishaNdiyoHaya
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1