“You’ll more quickly find an earthly thing kept from the earth than you will a person cut off from other human beings.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 9.9.3
Ni bahati iliyoje kwa kila mmoja wetu aliyeweza kuiona siku hii mpya ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TUNATEGEMEANA…
Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, tunategemeana sana ili kuweza kupiga hatua kwenye maisha yetu.
Hakuna mtu mmoja anayeweza kufanya kila kitu peke yake, kila mmoja wetu anawategemea watu wengine wengi katika maisha yake.
Kwa kuwa watu wengine ni muhimu sana kwetu, tunapaswa kuwajali sana wengine.
Tunapaswa kuhakikisha chochote tunachofanya, kina mchango bora kwa wengine.
Kufanya chochote chenye madhara kwa wengine ni kuchagua kujidhuru wewe mwenyewe.
Lakini pia unakuwa umeenda kinyume na kanuni ya asili, na hivyo unatengeneza madhara zaidi ya baadaye.
Kujifunza falsafa kunatupa nafasi ya kuijua asili ya binadamu kwa undani.
Na unapoijua asili hii, una hatari ya kuwadharau wengine, hasa pale wanapofanya makosa ya wazi, na kujiona wewe ni bora zaidi.
Lakini unapaswa kuzuia hilo lisitokee kwako, hata kama mtu mjinga au mpumbavu kiasi gani, kuna manufaa aliyonayo kwako.
Hivyo una wajibu wa kutengeneza mahusiano bora na wale wote wanaokuzunguka kwa sababu unawahitaji sana ili kuweza kupiga hatua.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutambua mchango wa wengine kwenye maisha yako, hata wale unaoona hawana maana. Wote wana mchango mkubwa kwa mafanikio yako.
#TumeumbwaKutegemeana #HakunaJeshiLaMtuMmoja #JaliKuhusuWengine
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1