“Our rational nature moves freely forward in its impressions when it:
1) accepts nothing false or uncertain;
2) directs its impulses only to acts for the common good;
3) limits its desires and aversions only to what’s in its own power;
4) embraces everything nature assigns it.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.7

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii mpya tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari TABIA NNE ZA USTOA…
Marcus Aurelius anatukumbusha tabia nne za Ustoa ambazo tunapaswa kuzizingatia na kujipima nazo kila siku.
1. Kubaliana na ukweli pekee. Usikubaliane na kitu kwa sababu wengi wanakubaliana nacho, bali kubali kile ambacho ni kweli, bila ya shaka yoyote.
2. Fanya kazi yenye manufaa kwako na kwa wengine pia. Usijiangalie wewe tu unapata nini, bali angalia wengine pia wananufaikaje na kile unachofanya.
3. Weka mahitaji yako kwenye mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako wa kuyadhibiti. Usisumbuke na mambo ambayo yako nje ya uwezo wako kudhibiti.
4. Pokea kile ambacho asili imeleta kwako, usishindane na asili, siku zote asili huwa inashinda.

Ukiziandika tabia hizi nne na kuzikariri na kila siku ukawa unajikumbusha, utajiepushia matatizo na changamoto nyingi ambazo umekuwa unakabiliana nazo mara kwa mara.
Angalia kila changamoto unayopitia sasa na ona kama hakuna tabia moja au zaidi ambayo uliivunja na kusababisha changamoto hiyo.
Kama upo kwenye madeni ni kwa sababu unakazana na mambo ambayo yako nje ya uwezo wako.
Kama hupendi kazi au biashara unayofanya ni kwa sababu unajiangalia wewe zaidi kuliko wengine.
Ukizingatia tabia hizi nne, utakuwa na maisha bora na tulivu wakati wote.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuziishi tabia hizi nne za ustoa, kukubali ukweli, kufanya kazi yenye manufaa, kuhangaika yaliyo ndani ya uwezo wako na kupokea kile ambacho asili imeleta kwako.
#IshiKistoa #MsingiNiMuhimu #JitathminiKilaSiku

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1