“How satisfying it is to dismiss and block out any upsetting or foreign impression, and immediately to have peace in all things.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.2
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari HAMISHA AKILI YAKO…
Unajua kabisa ni vitu gani ukivifikiria vinakuletea hasira, wivu ma chuki,
Unajua kabisa ni mazungumzo gani yakianza unapokuwa na wengine yanaleta mabishano makali.
Unajua kabisa ni mazungumzo ya aina gani ukiyafanya wewe na mwenza wako huwa mnaishia kutokuelewana au kugombana.
Pamoja na kujua hayom bado unaruhusu hali hizo zitokee, unakuwa unategemea nini?
Ukishajua fikra na mazungumzo ambayo huwa hayaishii vizuri, ni wajibu wako kuachana nayo mara moja pale yanapoanza.
Ukishaona mawazo au mazungumzo hayo yanaanza, hamisha akili yako, ondoka kwenye eneo hilo, badili aina ya mazungumzo.
Hii ni njia bora ya kujiepusha na yale yanayokukwaza na kukuvuruga,
Na hakuna chochote unachopoteza kwa kujiondoa kwenye hali zinazokupeleka kuvurugwa.
Ukawe na siku bora sana ya leom siku ya kutambua haraka aina ya mawazo na mazungumzo ambayo huwa hayaishi salama kwako na hivyo kuachana nayo mapema kabla hayajafika mbali.
#UnajuaKinachokuvuruga #ZuiaKablaHakijaletaMadhara #KingaNiBoraKulikoTiba
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania