“You are afraid of dying. But, come now, how is this life of yours anything but death?”
—SENECA, MORAL LETTERS, 77.18

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu tumeipata leo, kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UNAHOFIA KUPOTEZA NINI?
Unapohofia kifo, unachohofia kupoteza ni nini?
Maana watu wengi sana wamekuwa wanahofia kifo, wamekuwa wanatamani sana kuishi miaka mingi, lakini ukiangalia wanachofanya na maisha yao, unapata sikitiko.

Unahofia kifo halafu unapoteza masaa ya siku kuangalia tv, kuzurura mitandaoni, kufuatilia maisha ya wengine na udaku, kwenda kwenye kazi usiyoipenda, kugombana na watu na mengine mengi.
Je hayo ndiyo unayohofia kupoteza kila unapohofia kifo?
Kama jibu ni ndiyo basi unajidanganya, kwa sababu unahofia kifo huku ukichagua kuyapoteza maisha yako kwa mambo yasiyokuwa na maana kabisa.

Kama kweli unahofia kifo, kama kweli unayajali maisha yako, hebu onesha hilo kwenye kila unalofanya kwenye muda wa maisha yako.
Usipoteze muda wako kwa mambo ambayo hayana msingi wowote kwako, mambo ambayo hayaachi alama yoyote pale unapoondoka.
Maana kuishi maisha ya kupoteza muda, hayana tofauti na mtu ambaye ameshakufa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuishi maisha yanayitofautiana na aliyekufa, kwa kufanya mambo ambayo yataacha alama hapa duniani.
#ThaminiMaishaYako #JaliMudaWako #UsihofieKifoHofiaKutokuishi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani
http://www.t.me/somavitabutanzania