“It’s a disgrace in this life when the soul surrenders first while the body refuses to.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.29

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIKUBALI ROHO IWE YA KWANZA KUSHINDWA…
Usikubali roho yako iwe ya kwanza kushindwa,
Usikate tamaa haraka wakati bado mwili una nguvu,
Endelea na mapambano bila ya kujali ni kitu gani unapitia.
Kama bado una mwili, basi una kila sababu ya kuendelea na mapambano.

Kuwa imara kiroho, kuwa na matumaini kwamba utaweza kufanya makubwa na chukua hatua bila ya kuwa na wasiwasi wala kukata tamaa.
Safari hii siyo rahisi, ila inawezekana kama umejitoa kweli.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutokukata tamaa, siku ya kuendelea na mapambano mpaka kieleweke.
#RohoIweHamasaKwaMwili #EndeleaNaMapambano #UsikateTamaa

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani
http://www.t.me/somavitabutanzania