“Stop wandering about! You aren’t likely to read your own notebooks, or ancient histories, or the anthologies you’ve collected to enjoy in your old age. Get busy with life’s purpose, toss aside empty hopes, get active in your own rescue—if you care for yourself at all—and do it while you can.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 3.14
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUSOMA HAKUTAKUSAIDIA KAMA HUCHUKUI HATUA…
Kusoma vitabu kuna manufaa kwako kama utachukua hatua kwenye yale ambayo umejifunza.
Lakini kama hutachukua hatua, kusoma kwako hakutakuwa na msaada wowote.
Hivyo kwa kila unachojifunza, jiulize unawezaje kukitumia kwenye maisha yako na kisha kitumie mara moja.
Unapojikuta kwenye magumu au changamoto, jiulize ni maarifa gani ambayo ulishapata huko nyuma ambayo yanaweza kukusaidia kwa hali unayopitia.
Kumbuka kwamba wewe pekee ndiye mwenye wajibu wakujiokoa mwenyewe, hakuna mwingine atakayekuja kufanya hivyo.
Hivyo basi, kwa kila unachosoma na kujifunza, angalia namna unavyoweza kukitumia kwenye maisha yako na yakawa bora zaidi.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuyatumia yale yote ambayo umejifunza ili uweze kuwa na siku bora sana na kukabiliana na changamoto mbalimbali.
#KujifunzaPekeeHaitoshi #WekaKwenyeMatendo #JiokoeMwenyewe
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania