“The life of a person without faith is the life of an animal.” – Leo Tolstoy

Tofauti yetu sisi binadamu na mbuzi ni uwezo wetu wakufikiri na kufanya maamuzi kulingana na hali tunayopitia.
Wanyama wengine wanaendeshwa na mazingira na miili yao, lakini sisi binadamu tunaweza kudhibiti mazingira na miili yetu kulingana na kile tunachotaka.

Lakini pia binadamu tuna nguvu nyingine kubwa sana ambayo wanyama hawana.
Ni nguvu ya imani, kuamini kwenye kitu kikubwa kuliko sisi, kuwa ma matumaini kwamba mambo yatakuwa bora kuliko yalivyo sasa.
Ni nguvu hii ya imani ambayo imetuwezesha binadamu kuwa na ndoto kubwa za kwenda nje ya sayari hii ya dunia, wakati wanyama wengine wakiendelea na maisha ambayo wamekuwa nayo miaka yao yote.

Hivyo rafiki, unapoimaliza siku ya leo, jiulize ni kwa namna gani umeiishi siku hii tofauti na mnyama.
Je leo umetumia uwezo wako wa kufikiri katika kufikiri na kufanya maamuzi sahihi?
Je leo umetumia nguvu kubwa ya imani iliyopo ndani yako kuweza kuwa na matumaini makubwa kwenye ndoto uliyonayo na kujisukuma ili kuifikia?

Kuwa mtu wa kufikiri kwa usahihi, kuwa mtu wa imani na maisha yako yatakuwa bora sana hapa duniani.
Jitofautishe na wanyama kwa kutumia vyema nguvu hizo mbili ulizonazo.

Ukawe na wakati mwema, ukaipangilie siku inayofuata ili uweze kuishi kama binadamu na siyo kama mnyama.

Kocha.