“We have to fulfill honestly and irreproachably the work destined for us. It does not matter whether we hope that we will become angels some day, or believe that we have originated from slugs.” —JOHN RUSKIN
Asubuhi njema mwanamafanikio.
Kitu kimoja unachopaswa kujua ni kwamba, haupo hapa duniani kwa bahati mbaya.
Lipo kusudi la wewe kuwepo hapa duniani.
Na maisha yako yatakamilika pale utakapolijua na kuliishi kusudi la maisha yako.
Jukumu lako la kwanza hapa duniani ni kulijua kusudi lako kisha kuliishi kila siku ya maisha yako.
Kwa kufanya kile ambacho ni kusudi lako, hutaona kama ni kazi na utafurahia sana.
Utaona mchango mkubwa ambao unautoa kwa wengine na jinsi ambavyo maisha hao yanakuwa bora sana.
Asubuhi ya leo tafakari kusudi la maisha yako ni nini na umekuwa unaliishije kusudi hilo kila siku ya maisha yako.
Kama kazi au biashara unayofanya inatokana na kusudi pa maisha yako, basi uko pazuri.
Lakini kama bado hujaanza kuliishi kusudi la maisha yako, anza kidogo kidogo, kwa kila siku kufanya kitu ambacho kipo kwenye kusudi lako.
Ukiliishi kusudi lako, umeyaishi maishs yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania