“Kind people help each other even without noticing that they are doing so, and evil people act against each other on purpose.” —CHINESE PROVERB

Siku nyingine mpya ipo mikononi kwetu.
Maamuzi ni yetu kwa namna tunavyokwenda kuitumia siku hii.
Ni muhimu tuwe na vipaumbele sahihi ili kuweza kufanya makubwa kwenye siku hii.

Watu wema na watu waovu wana tofauti moja kubwa sana.
Watu wema wanasaidiana bila hata ya kujua, lakini watu waovu wanafanyiana mabaya kwa makusudi kabisa.

Kufanya wema ni kitu ambacho kipo ndani ya mtu, na wale walio wema wapo tayari kufanya wema hata kabla ya kuulizwa, wakati mwingine hawajui hata kama wanafanya wema, wameshazoea kufanya hivyo.

Kufanya ubaya pia ni kitu ambacho kipo ndani ya mtu, wale walio waovu huwa hawapendi kuona wengine wakifanikiwa, hivyo kwa makusudi huwa wanafanya mambo ya kuwazuia wengine wasiweze kupiga hatua.

Jukumu lako kwenye maisha ni kuwa mtu mwema, kupenda mafanikio ya wengine na hivyo kuwa tayari kuwasaidia wengine ili wapige hatua zaidi.
Pia wajue wale ambao ni waovu na waepuke kwenye maisha yako, maana watu hao huwa hawarekebishiki.

Sisi binadamu ni kitu kimoja, tunaweza kufanikiwa pale tu tunaposhirikiana na kusaidiana, kinyume na hapo wote tunaangamia.
Nenda katende wema leo na kila siku ya maisha yako, na wengine watakuwa tayari kukutendea wema pia.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania