A gunshot wound may be cured, but the wound made by a tongue never heals. —PERSIAN WISDOM

Kidonda kinachosababishwa na kisu, mshale au risasi kinaweza kupona na hata mtu kusahau kabisa kuhusu kidonda hicho.
Lakini kidonda kinachosababishwa na ulimwi, huwa hakiponi kamwe.
Hivyo kabla hujatoa neno lolote lichuje kwanza, kwa sababu neno likishatoka huwezi kulirudisha.
Kuongea hovyo kuna madhara makubwa sana kwako na kwa wengine pia.
Hivyo chunga sana ulimi wako, hakikisha unachokitoa ni kweli na upo tayari kukisimamia.

Tafakari wakati unaimaliza siku hii ya leo, ni jinsi gani umeutumia ulimi wako kwenye siku hii.
Je umejenga daraja au umetengeneza kidonda kisichopona?
Kwa jibu utakalopata, chukua hatua sahihi.

Kocha.