Who is a good man? Only a man who has faith is good. What is faith? This is when your will is in consent with the world’s conscience and the world’s wisdom. —CHINESE PROVERB

Tumeiona siku hii nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni siku ya kwenda kufanya yale yaliyo muhimu kwetu ili tuweze kupiga hatua zaidi.

Mtu mwema ni yule mwenye imani kwenye wema.
Na imani ni pale matakwa yako yanapoendana na dhamira pamoja na hekima ya dunia.

Kutaka kitu ambacho asili haiwezi kukupatia ni kujidanganya.
Kutaka kitu halafu usiwe tayari kuweka kazi ili kukipata ni kujidanganya pia.

Wema ni kuishi kulingana na asili na watu wema wanaishi kwa misingi ya asili.
Hawalazimishi mambo yasiyowezekana,
Wala hawategemei matokeo bila ya kuweka kazi.

Chagua kuwa mwema na uishi kwa misingi ya asili leo na kila siku ya maisha yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania