“A person should not think too much about what will happen after his life. Follow the will of those who sent us into this world; that will is in our minds and our hearts.” -Leo Tolstoy

Kuiona siku hii nyingine mpya ya leo ni nafasi ya kipekee sana kwetu.
Tumepata bahati kuiona siku hii, hivyo tunapaswa kwenda kuitumia vizuri ili kuweza kupata matokeo bora wana.

Hupaswi kujisumbua na kifo,
Kujiuliza kila mara kwamba nini kitatokea kwako baada ya kifo chako hakukusaidii kuyaishi maisha yako vizuri leo.
Badala yale kazana kuishi maisha bora sana leo, kama vile leo ndiyo siku yako ya mwisho kuwa hapa duniani.
Kuishi kile kilichopo ndani yako ndiyo namna bora ya kuyaishi maishs yako.

Usijisumbue sana kuhusu kifo, kwamba kitakuja kwako wakati gani na nini kitatokea kwako baada ya kifo.
Kusumbuka na hayo ni kukosa muda wa kuyaishi maisha yako.
Wewe ishi maisha bora leo na kama utapata siku nyingine kesho, ipokee kama zawadi na ishi maisha bora kwenye siku hiyo pia.
Iishi kila siku kama inavyokuja, iishi kwa ubora na utaweza kuwa na maisha mazuri sana, bila ya kujali kama ni mafupi au marefu.

Wote tunajua kwamba hakuna atakayetoka hapa duniani akiwa hai,
Lakini hatuijui siku yetu ya kutoka hapa duniani ni lini.
Hivyo hatupaswi kujisumbua na siku hiyo,
Bali tunapaswa kusumbuka kuiishi vyema siku hii ya leo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania