“Seneca, a wise man from Rome, said that when you want to escape from your rage, when you feel that it grows, the best thing to do is to stop. Do not do anything: do not walk, do not move, do not speak. If your body or your tongue moves at this moment, then your rage will grow.” – Leo Tolstoy

Tumepata nafasi nyingine nzuri ya kuiona siku hii mpya ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.

Mwanafalsafa Seneca anatuambia, unapokuwa na hasira, usifanye chochote.
Usitembee, usiongee wala usifanye chochote.
Badala yake pumzika kwanza,
Na kuhakikisha hufikirii kile kilichokupa hasira, fanya zoezi la kuhesabu.
Hesabu mpaka kumi, kama bado utakuwa na hasira, hesabu mpaka mia, kama bado ipo hesabu mpaka elfu moja.

Kuna mambo mengi tunakutana nayo kwenye maisha na yanatupa hasira,
Lakini yote hayo hayana madhara kwetu mpaka pale tunapofanya au kusema kitu tukiwa na hasira.
Hapo ndipo tunasababisha madhara makubwa kwetu na kwa wengine pia.

Kitu sahihi kufanya unapokuwa na hasira ni kutokufanya chochote.
Maana hakuna utakachofanya ukiwa na hasira kikakuacha salama.
Huwezi kuzuia hasira isikuingie, maana hizo ni hisia ambazo zinaweza kuibuliwa na mambo mengi.
Ila unaweza kuzuia hasira inayokuingia isiwe na madhara makubwa kwako, kwa kujizuia usifanye chochote unapokuwa na hasira.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania