“An evil person damages not only others but himself.” —After SOCRATES

Unaweza kufanya ubaya kumlenga mtu mwingine, lakini jua kwamba ubaya huo utakuwa na madhara kwako kuliko kwa unayemfanyia.
Kadhalika kwa yule anayekufanyia ubaya, tambua unamdhuru zaidi yeye mfanyaji kuliko wewe mfanyiwaji.
Kwa kujua hili, tujiepushe kuwafanyia wengine mabaya,
Na pia kwa wale wanaojaribu kutufanyia ubaya, tuwaonee huruma.

Tindikali huanza kutaunguza chombo ambacho kimeubeba,
Na wewe usiwe chombo kinachobeba mabaya na maovu, kwa sababu yatakuharibu wewe mwenyewe.

Uwe na wakati mwema, wakati wa kujitafakari kwa pale ulipoteleza na kufanya mabaya na kuhakikisha hurudii tena.
Kocha.