“Experience teaches only the teachable.” —Aldous Huxley
Wanasema uzoefu ni mwalimu mzuri,
Kwamba kile unachofanya na kupata matokeo fulani, unajifunza na kufanya kwa ubora zaidi au kutokufanya wakati mwingine.
Lakini vipi wale ambao wanarudia makosa yale yale kila mara,
Wale ambao kila wakati wapo kwenye madeni,
Wale ambao kila biashara wanayoanzisha inakufa,
Wale ambao kila kazi wanayopata wanafukuzwa,
Wale ambao hawadumu kwenye mahusiano kwa muda mrefu,
Je hawa hawapati uzoefu?
Jibu ni uzoefu wanaupata sana, ila kwa sababu hawafundishiki, basi uzoefu huo unakuwa hauna maana kwao.
Swali ni je watu wasiofundishika na uzoefu ni wa aina gani?
Ni wale ambao wanaamini wako sahihi mara zote.
Wale ambao kila kinachotokea wanalalamika na kulaumu wengine.
Wale ambao wanajiambia wana bahati mbaya.
Wale ambao wanaamini kuna watu wanawazuia wasipige hatua.
Uzoefu unawafundisha wale ambao wanafundishika, je wewe ni mmoja wa wale wanaofundishika?
Tafakari hilo usiku wa leo, na unapokwenda kuianza kesho, iwe ni kwa namna ambayo kila uzoefu unaoupata unakuwa darasa kwako.
Kocha.
Nimekelewa vinzuri Sana kocha
Kila siku najifunza kitu muhimu natakiwa kuweka nidhamu ya kufanya kwa vitendo
LikeLike