Rafiki yangu mpendwa,

Hivi bado tunauita mwaka huu 2020 mpya? Kwa sababu ndani ya mwezi huu wa kwanza wa mwaka huu, katika watu 10 walioweka malengo, 7 wameshayasahau kabisa na wamerudi kwenye mazoea yao. Na watatu waliobaki, wawili wana wasiwasi juu ya malengo yao na mmoja ndiyo bado anaendelea na malengo yake kama alivyoyaweka.

Sijui wewe upo kundi gani katika hayo, unajua mwenyewe, lakini wanasema namba hazidanganyi. Tafiti zimekuwa zinaonesha hivyo, kwamba katika wiki tatu za kwanza kwenye mwaka, asilimia 90 ya watu wanakuwa wameshaachana na malengo yao na kurudi kwenye mazoea.

goals 2020.jpg

Tarehe moja ya mwezi wa kwanza kila mtu anakuwa anashangilia mwaka mpya mambo mapya, halafu kila mtu anaorodhesha mambo makubwa atakayofanya kwenye mwaka husika.

Tarehe ishirini na ya mwezi wa kwanza, wengi wanakuwa wamesharudi kwenye mazoea yao, ule upya wa mwaka wameshausahau huku malengo yao wakiona kama hayawezekani.

Rafiki, leo nakwenda kukupa sababu moja kwa nini hutayafikia malengo uliyojiwekea kwa mwaka huu 2020. Kama kweli umejitoa kuhakikisha unafikia malengo hayo, ni vyema ukajua sababu hii na jinsi ya kuivuka.

Kwenye makala hii nakwenda kukupa ukweli kama ulivyo, ukweli ambao huenda utakuumiza, hivyo kuwa tayari kukabiliana na ukweli hii muhimu kuhusu wewe ili uweze kupiga hatua.

—————————————————————————————————

Moja ya bahati kubwa ambazo nimezipata kupitia huduma mbalimbali za ushauri na ukocha ninazotoa, ni kuweza kuzijua tabia za watu kwa karibu kabisa.

Kupitia ushauri, mwongozo na hata ukocha ninaotoa kwa watu mbalimbali, nimekuwa naona tofauti kubwa sana ya matokeo ambayo watu wanazalisha wakiwa na usimamizi wa karibu kuliko wakiwa wao wenyewe.

Watu wengi wamekuwa wanaweza kufanya makubwa wakiwa na kwenye programu mbalimbali za ukocha, siyo kwa sababu programu hizo zinaongeza kitu chochote kwao, bali ni kwa sababu zinawanyima sababu ya kutekeleza tabia pendwa kwa kila mtu, ambayo ni kuahirisha mambo.

—————————————————————————————————-

Rafiki, kwa asili, sisi binadamu ni viumbe wavivu sana, huwa hatupendi kutumia nguvu zetu kwa jambo lolote lile. Ubongo wetu umetengenezwa kwa namba ambayo kipaumbele kwake ni kutunza nguvu kwa ajili ya kufikiri au kuchukua hatua pale kunapokuwa na hatari.

Ndiyo maana unapokuwa umepanga kufanya kitu, halafu unafika wakati wa kuchukua hatua, huwa hukosi sababu ya kuchelewa kidogo kuchukua hatua. Utajiambia hujawa tayari, utajiambia unapaswa kusubiri na mengine mengi.

Unaweza kupata mfano mzuri kwenye kuamka mapema asubuhi, unaweka alamu kabisa kwamba ikilia unaamka. Kweli inalia, na unastuka, lakini unajiambia wacha ulale kwa dakika 5 tu na utaamka, unakuja kuamka masaa mawili baadaye. Hivi unafikiri kabisa dakika 5 za ziada zinaweza kukupa usingizi wenye maana kwako? Hiyo ni njia ya akili yako kukutega, ili uingie kwenye mtego wake wa kupumzika zaidi na siyo kufanya kazi.

Lakini pata picha, tayari una tiketi ya ndege, ambayo inaondoka mapema na umeweka alamu ya kukuamsha mapema, alamu ikiita tu, hupotezi hata sekunde moja kitandani. Tena wakati mwingine utaamka kabla hata ya alamu.

Sasa rafiki hebu jiulize tofauti hapo ni nini, mtu ni wewe wewe, lakini kwenye hali moja unashindwa kuamka mapema, huku kwenye hali nyingine ukiweza kuamka bila ya shida?

Ukipata jibu la swali hilo, basi umeshaelewa somo la leo na umeshapata sababu kwa nini hutafikia malengo uliyojiwekea mwaka huu 2020.

Rafiki, sababu kuu itakayokuzuia kufikia malengo uliyojiwekea mwaka huu 2020 ni kukosa mtu wa kukusimamia kwenye malengo hayo.

Kama umejiwekea malengo hayo wewe mwenyewe na unayafanyia kazi peke yako, ni swala la muda tu, hutafika nayo mbali. Kwa sababu kwa lengo lolote unalojiwekea, kuna wakati wa kujaribiwa, ambapo utakutana na magumu au changamoto ambazo zitakuangusha kabisa.

Sasa unapofika kwenye hatua hiyo, kama lengo hilo umejiwekea mwenyewe, kama hakuna mtu mwingine anayekusimamia kwenye lengo hilo, akili yako inafanya yake. Inakuambia huna haja ya kujitesa, inakuambia kuna mambo mengine rahisi ya kufanya, na hicho ndiyo kinakuwa kifo cha malengo yako.

Haijalishi una akili kiasi gani, haijalishi una hamasa kiasi gani, akili yako ni janja kuliko wewe, na kwa sababu haitaki kuumia au kupoteza nguvu, ukiwa peke yako, ni rahisi sana kukata tamaa na kuishia njiani.

Hivyo rafiki yangu, unahitaji mtu wa kukusimamia kwenye malengo unayojiwekea kama kweli unataka kuyafikia. Mtu ambaye hatakuonea huruma au kukubaliana na wewe kirahisi pale unapotaka kuachana na malengo yako. Mtu ambaye atakuambia wazi pale unapokosea au kutoka nje ya malengo yako.

Kwa bahati mbaya sana, jamii yetu ina upungufu wa watu hawa, kwa sababu watu wengi kwenye jamii hawawezi kufikia malengo waliyojiwekea wao wenyewe, hivyo hawawezi kujiamini kuwasimamia wengine nao wafikie malengo yao. Hivyo hata unapowaomba wakusimamia, ni rahisi kukuachia pale unapoanza kulegalega.

Njia bora ya kupata mtu wa kukusimamia kwenye malengo yako ya 2020.

Rafiki, umeshaona sababu kubwa itakayokuzuia kwenye malengo yako ni kukosa mtu wa kukusimamia.

Lakini pia umeona kwamba kwenye jamii zetu kuna uhaba wa watu wanaoweza kutusimamia.

Hii inakuweka njia panda, je huna namna ya kupata mtu sahihi wa kukusimamia kwenye malengo yako ili mwaka huu 2020 uwe wa tofauti na wa kipekee kwako?

Jibu ni ipo njia bora kwako kupata mtu wa kukusimamia kwenye malengo yako kwa mwaka huu 2020.

Na njia hiyo ni kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na kuchukua hatua kwenye miongozo mbalimbali ambayo inatolewa.

Moja ya mambo tofauti kwa mwaka huu 2020 kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni kwamba unanishirikisha mimi kocha wako lengo lako kuu la mwaka 2020 pamoja na kipato cha ziada unachokwenda kutengeneza kwenye mwaka huu. Baada ya hapo, kila mwezi ninakuwa nakuuliza unaendeleaje na lengo lako la mwaka. Na hapo unapaswa kunishirikisha maendeleo, pamoja na ushahidi kwamba unafanya kweli.

Lakini pia kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, unapata nafasi ya kujiunga na klabu za KISIMA CHA MAARIFA, hivyo nguvu hii ya kufuatiliwa haiwi tu kwenye mtandao, bali unakutana ana kwa ana na watu wenye kiu ya mafanikio kama wewe, ambao utawashirikisha malengo yako, na kila mwezi mnakutana pamoja na kushirikishana hatua ambazo kila mtu anaendelea kupiga kwenye malengo hayo.

Kwa nguvu hizi mbili, kuwa na kocha ambaye anakufuatilia kila mwezi, na kuwa na watu ambao wapo karibu yako na wanakufuatilia, lazima utafikia malengo yako uliyojiwekea 2020. Na hata kama hutayafikia, basi utapata matokeo bora 2020 kuliko matokeo ambayo umewahi kupata huko nyuma.

Na kama tayari upo kwenye KISIMA CHA MAARIFA, kuna huduma nyingine za ukocha kama LEVEL UP (ambapo ufuatiliaji ni wa kila wiki) na GAME CHANGERS (ambapo ufuatiliaji ni wa kila siku) ambazo unaweza kujiunga nazo na ukazidi kupata manufaa ya kuwa na mtu wa kukufuatilia kwenye malengo yako.

Watu wanatengeneza matokeo makubwa sana kwenye programu hizo, matokeo ambayo wao wenyewe wanakiri wasingeweza kuyatengeneza kama wangekuwa peke yao. Watu wanajisukuma licha ya kukutana na changamoto kubwa, kwa sababu wanajua wanapaswa kutoa mrejesho wa kile walichofanya.

Karibu kwenye huduma hizi.

Rafiki, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi zawadi kubwa na ya kipekee unayoweza kujipa mwaka huu 2020 ni kuwa mwanachama. Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii ili upate nguvu hii ya kufuatiliwa kwa karibu, ambayo itakusukuma ufikie malengo yako. wekeza tsh laki moja (100,000/=) ambayo ni ada ya mwaka na utaweza kupata manufaa makubwa sana kwa mwaka mzima ambao tutakuwa pamoja. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ujumbe kwenda wasap namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA na utapewa maelekezo zaidi.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi fanya haya;

Moja; hakikisha unajibu taarifa za kujitathmini za kila mwezi, ambapo kupitia taarifa hizi utashirikisha lengo lako kuu na hatua unazochukua kulifikia. Kwa hakika mwaka huu 2020 sitakuacha nyuma, nitakufuatilia mpaka ufanye au ukimbie kabisa, usitake hata kuniona.

Mbili; kama una biashara, basi jiunge na programu ya LEVEL UP, hii ni programu maalumu ya kupiga hatua kwenye biashara yako, nafasi zipo chache kwa wale wanaohitaji.

Tatu; kama kuna kitu cha tofauti umekuwa unataka kufanya kwenye maisha yako lakini unashindwa kuanza au unaahirisha kila mara, basi karibu kwenye programu ya GAME CHANGERS. Kwa sasa tunaendelea na msimu wa JANUARI 2020 ambapo watu wanajisukuma na kufanya makubwa sana. Msimu unaofuata ni wa MACHI 2020, hivyo kama unataka kushiriki programu hii kwenye msimu huo, wahi nafasi sasa. Nafasi za kushiriki programu hii ni tano tu kwa wakati mmoja.

Kujiunga na programu hizi, tuma ujumbe kwa wasap kwenda namba 0717396253 wenye jina la programu, yaani LEVEL UP au GAME CHANGERS na utapewa maelekezo ya kujiunga. Angalizo, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA kwanza ndiyo unufaike na programu hizo.

Rafiki yangu mpendwa, kataa kabisa mwaka 2020 kuwa kama miaka ya nyuma, tumia fursa hizo nilizokushirikisha ili uweze kufanya makubwa sana. Nipo hapa kwa ajili yako, karibu twende pamoja safari hii ya kuelekea mafanikio makubwa.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania