“You can achieve wisdom in three ways. The first way is the way of meditation. This is the most noble way. The second way is the way of imitation. This is the easiest and least satisfying way. Thirdly, there is the way of experience. This is the most difficult way.” —CONFUCIUS
Hongera sana kwa kupata nafasi hii nyingine nzuri ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.
Tuweke vizuri vipaumbele vyetu na tuvifanyie kazi.
Kuna njia tatu za kupata hekima,
Njia ya kwanza ni kupitia tahajudi, ambayo ndiyo njia bora kabisa ya kupata hekima.
Njia ya pili ni ya kuiga, kujifunza kutoka kwa wengine. Hii ni njia rahisi lakini isiyoridhisha.
Njia ya tatu ni kupitia uzoefu binafsi, ambayp ndiyo njia ngumu kuliko zote.
Kila mmoja wetu anaweza kufanya tahajudi, na hekima ya dunia ikafunuliwa kwake kwa njia hiyo ya tahajudi.
Lakini pia hakuna ubaya kujifunza kupitia wengine, yale mazuri wanayofanya na kupiga hatua na yale mabaya wanayofanya na kuwakwamisha.
Huhitaji kujifunza kila kitu kwa uzoefu wako mwenyewe, kwa kujaribu na kushindwa.
Ni njia ngumu, ndefu na yenye maumivu.
Tumia njia mbili za kwanza kupata hekima na maisha yako yatakuwa bora sana.
Ukawe na siku bora kabisa leo, siku ya kupata hekima kupitia tahajudi na kujifunza kwa wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania