“You should respond with kindness toward evil done to you, and you will destroy in an evil person that pleasure which he derives from evil.” – Leo Tolstoy
Tumeiona siku nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.
Mtu anapokufanyia ubaya, anategemea uumie, ukasirike na ujaribu kulipa ubaya huo kwa ubaya.
Hivyo anayekufanyia ubaya anapoona unalipa kwa ubaya, lengo lame linakuwa limekamilika, alichokitaka kimefanikiwa.
Lakini mtu anapokufanyia ubaya halafu wewe ukamjibu kwa wema, unammaliza nguvu kabisa.
Alichotegemea ufanye hujafanya,
Hilo linamfanya ajidharau sana na akose sababu ya kuendelea kukufanyia ubaya.
Usikubali kuingia kirahisi kwenye mtego wa watu waovu, ambao wanakifanyia ubaya ili na wewe ujibu kwa ubaya.
Badala yake wapuuze, chukulia kama hujaona wala kusikia walichofanya.
Na nafasi inaporuhusu, wajibu kwa wema.
Hapo unakuwa umewakaanga kwa mafuta yao wenyewe,
Wataumia sana kwa jinsi ulivyoweza kuvuka ubaya wao huo,
Wewe unakuwa juu na wao wanakuwa chini.
Watu wengi wanakutega kwa nia zao mbalimbali,
Chunga sana usiingie kwenye mitego hiyo.
Uwe na siku bora leo, siku ya kujibu ubaya kwa wema na kuwashinda wale wote wanaokutega kwa manufaa yao wenyewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania