“Love is real only when a person can sacrifice himself for another person. Only when a person forgets himself for the sake of another, and lives for another creature, only this kind of love can be called true love, and only in this love do we see the blessing and reward of life. This is the foundation of the world.” – Leo Tolstoy
Upendo wa kweli ni kujitoa kwa ajili ya yule au wale unaowapenda,
Na siyo kutoa kwa sababu kuna kitu unategemea kupata.
Upendo wa kweli unajisahau wewe mwenyewe katika kuwahudumia wengine.
Upendo wa kweli ni pale unapoishi kwa ajili ya wengine, kuweka maslahi ya wengine mbele na siyo maslahi yako pekee.
Kabla hujalala leom jiulize je una upendo wa kweli?
Na je ni maeneo yapi kwenye maisha yako ambayo umekuwa unaishi kwa upendo wa kweli?
Unapoipanga kesho yako, ipange kuiishi kwa upendo wa kweli,
Kwenye kazi yako kuwa tayari kujitoa zaidi ya ulivyozoea,
Kwenye biashara yako weka maslahi ya wateja wako mbele.
Na kwenye mahusiano yako, jali kuhusu wengine kama unavyojijali wewe.
Jipende mwenyewe. Wapende wengine. Penda unachofanya.
Kocha Dr. Makirita Amani.