“Our thoughts, depending on whether they are good or bad, can bring us either to paradise or to hell; this happens, neither in heaven nor under the earth, but here, in this life.” —LUCY MALORY
Kuiona siku hii nyingine nzuri ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu.
Tuna fursa nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Pepo na jehanamu havipo mbinguni wala kuzimu,
Bali vipo ndani yako, kwenye fikra zako.
Kwa namna unavyofikiri, unaweza kuwa na maisha kama ya peponi ay ukawa na maisha kama ya kuzimu.
Fikra zako ndizo zinazoleta uhalisia kwenye maisha yako,
Unakuwa kile unachofikiri,
Hapo ulipo sasa ni matokeo ya fikra ambazo umekuwa nazo huko nyuma.
Fikra ulizonazo sasa ndiyo zinatengeneza matokeo ya kesho.
Unapaswa kuwa makini sana na fikra unazoruhusu ziingie na kutawala akili yako.
Hili ni eneo ambalo wengi wamepoteza udhibiti na hivyo kujikuta wanaruhusu kila mtu kuleta mawazo yake hasi kwao.
Fikra ndiyi kitu pekee ambacho una uhuru nacho kwa asilimia 100,
Na ndiyo kitu pekee kinachokuweka huru au kukufanya mtumwa.
Wale wanaotaka uwe mtumwa huwa wanaanza kuteka fikra zako, kukujaza hofu, kuondoa matumaini na kutengeneza utegemezi kwao.
Linda sana fikra zakom jijengee fikra chanya zinazokuletea pepo hapa duniani na zifute kabisa fikra hazi zinazokuletea jehanamu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania