“Remember how passionately you yearned in the past for many of the things which you hate or despise now.” – Leo Tolstoy

Tumepata nafasi nyingine mpya, nafasi bora na ya kipekee kwa kila mmoja wetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Kuna vitu ambavyo ulikuwa unavitamani sana siku za nyuma,
Ukajitoa na kujisukuma sana ili kuwa navyo.
Lakini baada ya kuwa na vitu hivyo, hujavifurahia kama ulivyofikiri.
Tena umevichukia kabisa na hata kuvidharau.

Katika hali kama hii, unakuwa umekubali kuendeshwa na tamaa zako, hasa tamaa za mwili au za kutaka kuonekana.
Tamaa ina nguvu kubwa ya kukusukuma, lakini huwa haikuridhishi baada ya kuikamilisha.
Vitu vingi unavyotamani huwa unaishia kuvidharau ukishavipata.

Ni muhimu sana kujua msukumo ulionao kwenye kupata kitu unatokana na nini.
Kama unatokana na tamaa, ni vyema kuachana nazo, maana tamaa hazijawahi kumridhisha yeyote.
Msukumo sahihi ni ule unaotokana na maamuzi ambayo mtu umeyafikia kwa fikra sahihi, ambazo hazijachafuliwa na tamaa.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kuendeshwa kwa fikra na siyo tamaa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania