“There is nothing more harmful to you than improving only your material, animal side of life. There is nothing more beneficial, both for you and for others, than activity directed to the improvement of your soul.” – Leo Tolstoy
Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kuendeleza mwili na kuisahau roho.
Mwili bila roho ni sawa na farasi mwenye mbio kali lakini asiye na dereva,
Anaishia kupoteza mbio zake kwa yasiyo na maana.
Roho yako ndiyp inayoongoza maisha yako,
Ipe kipaumbele sahihi kama unavyoupa mwili wako.
Hakuna siku unatembea uchi kimwili, lakini zipo siku nyingi unazotembea uchi kiroho.
Hakuna siku unaunyima mwili chakula au kinywaji cha aina yoyote, lakoni zipo siku nyingi ambazo unainyima roho chakula chake.
Chanzo cha matatizo mengi unayokumbana nayo, ni kuendeleza mwili na kusahau roho.
Ipe roho kipaumbele sahihi.
Uwe na usiku mwema,
Kocha Dr Makirita Amani