“The most powerful weapon known is the weapon of blessing. Therefore, a clever person relies on it. He wins with peace, not with war.” — LAO-TZU
Hongera sana rafiki kwa kuiona siku hii nyingine mpya ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwako kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Silaha yenye nguvu zaidi kuliko silaha nyingine zote ni baraka,
Utashinda mengi kwa kuwabariki watu na kwa amani kuliko kwa vita.
Utaepuka mengi kwa kutumia njia ya amani kuliko njia ya mabavu.
Hivyo mara zote tumia njia hii.
Baraka na amani,
Haijalishi uko kwenye hali gani, wabariki wengine,
Haijalishi nani mwenye makosa, tengeneza amani.
Usilipe ubaya kwa ubaya.
Mtu akikufanyia ubaya na wewe ukamjibu kwa ubaya, unakuwa umempa mtu huyo ushindi, maana ameweza kupandikiza ubaya ndani yako.
Lakini mtu akikufanyia ubaya na wewe ukambariki, ukamfanyia wema, unakuwa umeshinda, ubaya wake utakuwa moto utakaomchoma yeye mwenyewe.
Ataumia sana kwa majibu hayo ya amani kuliko ungemjibu kwa shari.
Unaona kwa nini baraka na amani ni silaha yenye nguvu?
Basi hakikisha unaitumia kila mara na kila wakati, hakuna ambapo silaha hii inashindwa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kushinda kila kitu kwa baraka na amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania