“To be strong, you have to be like water: if there are no obstacles, it flows; if there is an obstacle it stops; if a dam is broken, then it flows further; if a vessel is square, then it has a square form; if a vessel is round, then it has a round form. Because it is so soft and flexible, it is the most necessary and the strongest thing.” — LAO-TZU
Ni jambo la kushukuru sana kwa kupata nafasi hii nyingine nzuri ya leo.
Kwa kuonesha kweli kwamba unaithamini nafasi hii, unapaswa kuitumia vizuri, kwa kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.
Kama unataka kuwa imara, kuwa kama maji.
Maji ni imara kwa sababu hayatumii nguvu, badala yake yanabadilika kulingana na mazingira.
Kukiwa kuna upenyo yanapita, kusipokuwa na upenyo hayapiti.
Yakiwekwa kwenye kikombe yanakaa, kwenye chupa yanakaa, kwenye sahani yanakaa.
Huwezi kuyavunja maji, kwa sababu siyo magumu wala hayang’ang’ani na chochote.
Kuwa kama maji,
Unapoiona nafasi ya kufanya kitu fulani fanya,
Mazingira yanapobadilika na wewe badilika.
Usiwe mgumu, maana dunia huwa inapenda kuvunja vitu vigumu.
Kuwa mwepesi ili kuwa imara.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa kama maji, kwa kutumia kila nafasi unayoipata na kubadilika kulingana na hali au mazingira.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania