“When people speak in a very elaborate and sophisticated way, they either want to tell a lie, or to admire themselves. You should not believe such people. Good speech is always clear, clever, and understood by all.” – Leo Tolstoy

Ukweli ni rahisi na unaeleweka na wote,
Uongo ni mgumu na unahitaji maelezo marefu na yasiyo eleweka.
Hivyo hiki kinapaswa kuwa kipimo chako cha kwanza cha ukweli,
Kama kitu hakieleweki, kama mtu anakuelezea kitu kwa namna ambayo huelewi, basi jua kuna uongo au utapeli ndani yake.

Ukwa upande wako, chochote unachotaka kuwaambia au kuwashawishi wengine, kwanza hakikisha wewe unakielewa vizuri,
Halafu waeleze watu kwa lugha rahisi kwao kuelewa.
Mjinga yeyote anaweza kufanya mambo kuwa magumu (complicated)
Inahitaji akili sana kurahisisha mambo (simplified).

Mfano wa biashara ya kweli; nitanunua mchele kwa bei ya chini eneo A ambapo mchele unapatikana kwa wingi na kwenda kuuza kwa bei ya juu kwenye eneo B ambapo mchele haupatikani kwa wingi. Kila mtu anaelewa hilo.
Mfano wa biashara ya uongo; unapanda pesa zako hapa, halafu kila wiki unavuna faida, huhitaji kufanya kazi yoyote. Mambo yasiyoeleweka, pesa unazipandaje? faida inatoka wapi? Nini kinafanyika na fedha hizo?

Kumbuka, kama haieleweki, ni uongo au watu wanapanga kukutapeli,
Ukweli ni rahisi, uko wazi na unaeleweka.
Ukiona kitu kinapambwapambwa sana, kuwa makini.

Uwe na siku bora leo, siku ya kuepuka vitu visivyoeleweka na kuhakikisha chochote unachojihusisha nacho unakielewa vizuri na unaweza kuwaelezea wengine kwa urahisi na usahihi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania