“It is a sin not to be engaged in work, even if it is not necessary for you to make your living with everyday work.” Leo Tolstoy
Umewahi kujiuliza kwa nini naadhi ya watu hufa miaka michache baada ya kustaafu kazi?
Pamoja na sababu nyingine, kuna sababu moja kuu, asili kufanya kazi yake.
Iko hivi, unapokuwa na kazi za kufanya, asili inajua huyu mtu bado ana umuhimu na hivyo inakupa nafasi ya kuishi zaidi.
Unapokuwa huna kazi za kufanya, asili inajua mtu huyu ameshakamilisha maisha yake na hivyo inakuchukua.
Hivyo basi, kama unataka kuishi miaka mingi, hitaji la kwanza ni ufanye kazi kila siku.
Isifike siku ukajiambia umeshamaliza majukumi yote na sasa ni kupumzika na kustarehe.
Msamiati wa kustaafu uondoe kabisa kwenye maisha yako.
Kama upo hai, fanya kazi, hata kama huhitaji tena kutengeneza kipato cha kuendesha maisha yako.
Kazi haina mwisho, mwisho wa kazi ni kifo.
Ili uweze kufanya kazi kila siku ya maisha yako, bila kuchoka au kutamani kustaafu, lazima upende kile unachofanya, uwe na msukumo mkubwa ndani yako na siyo tu tamaa ya kupata fedha.
Kama unachofanya sasa ni kwa ajili ya kupata fedha, hakikisha kuna kingine unafanya pembeni ambacho unakipenda kweli, na pia unaweza kukitumia kuingiza fedha.
Utakapopumzika hicho unachofanya kwa ajili ya fedha tu, unaendelea na kile unachofanya kwa kupenda na kuingiza fedha pia.
Je ni kazi gani kwako haitakuwa na mwisho?
Jipe jibu la swali hili na liishi jibu hilo kila siku.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania