Niliwahi kukuambia kwamba ukitaka fedha zaidi basi toa thamani zaidi.
Leo nakuongezea kauli nyingine, ukitaka fedha zaidi, basi tafuta watu wengi zaidi wakuchukie.

Kwa nini?
Hii ni kwa sababu kama unataka kupata fedha zaidi, lazima ufanye tofauti na wengine wanavyofanya.
Na utakapofanya tofauti, watu wataanza kukuchukia,
Ndiyo maana chuki ni kipimo kizuri cha fedha.

Ili upate fedha zaidi lazima uwe na msimamo, watu wenye misimamo hawapendwi.
Ili upate fedha zaidi lazima uwe tayari kujitesa, watu wanaojitesa hawapendwi.
Kama unataka kila mtu akupende halafu pia ufanye makubwa, unajidanganya, hicho kitu hakipo.

Chuki za wengine ni mafanikio kwako,
Zisikuumize, badala yake zikukumbushe kwamba upo kwenye njia sahihi.

Kama hakuna anayekuchukia, ina maana kwamba;
👉🏼Hujawahi kuwa na msimamo kwenye kitu chochote.
👉🏼Hujawahi kusema Hapana kwa wengine.
👉🏼Hujawahi kupingana na wengi pale wanapokosea.
👉🏼Hujawahi kuwataka wengine wakulipe zaidi ya wanavyotaka wao.
👉🏼Hujawahi kuwa na malengo makubwa na kuwaambia watu waziwazi.

Uwe na usiku mwema, usiku wa kujua kwamba chuki za wengine ndiyo utajiri wako na hivyo kuzipokea na siyo kuzikwepa.

Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania