“If we wasted money the way we waste time, we’d all be bankrupt.” – Seth Godin

Kama ungekuwa unapoteza fedha kama unavyochagua kupoteza muda, basi ungekuwa umeshafilisika zamani sana.
Lakini ambacho hujui ni kwamba, kuchagua kupoteza muda ni kuchagua kupoteza fedha.

Hebu chukulia kwa kila dakika unayoipoteza ni tsh elfu moja umepoteza (au hata mia moja tu),
Kisha hesabu ni kiasi gani cha fedha unapoteza kila siku.
Muda unaobishana,
Muda unaozurura mitandaoni,
Muda unaofuatilia maisha ya wengine,
Muda unaotumia kufuatilia habari zisizo na umuhimu,
Zote hizo ni fedha umechagua kupoteza.

Upe muda wako thamani ya fedha, na kila unapopoteza muda, hesabu ni kiasi gani cha fedha umepoteza.
Ukiuangalia muda kwa mtazamo huo, utaujali na utaweza kufanya makubwa.

Uwe na usiku mwema, ukijiandaa kutumia muda wako wa kesho vizuri.
Kocha Dr Makirita Amani,