“Life is not given to us that we might live idly without work. No, our life is a struggle and a journey. Good should struggle with evil; truth should struggle with falsehood; freedom should struggle with slavery; love should struggle with hatred. Life is movement, a walk along the way of life to the fulfillment of those ideas which illuminate us, both in our intellect and in our hearts, with divine light.” —After GIUSEPPE MAZZINI

Kama mtu yeyote au wewe mwenyewe umewahi kujiambia kwamba maisha ni rahisi, umedanganywa au umejidanganya.
Maisha siyo rahisi, maisha ni mapambano na kadiri unavyojua na kujiandaa kwa hilo, ndivyo unavyoweza kufanya makubwa kwenye maisha.

Pambano muhimu kabisa kwenye maisha yako ni kazi, maisha hayawezi kwenda bila kazi.
Lazima kuwe na kitu unachofanya kinachoongeza thamani kwa wengine na wao kuwa tayari kukulipa.
Kazi ndiyo inakupa utu na heshima, penda sana kazi, ipe kipaumbele na kila wakati kazana kuwa bora kwenye kuifanya kazi yako.

Halafu kuna mapambano mengine madogo madogo ya kila siku;
Wema unapambana na uovu,
Ukweli unapambana na uongo,
Uhuru unapambana na utumwa,
Upendo unapambana na chuki,
Kama unavyojionea hapo, kila kitu ni mapambano, hivyo usipumzike na kuona maisha umeshayapatia,
Haya mapambano hayaishi mpaka siku unaondoka hapa duniani.

Nenda kapambane vyema leo, na kila siku ya maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania