“The question is not what you look at—but how you look & whether you see.” — Henry David Thoreau
Thoreau anatuambia swali siyo unaangalia nini, bali unaangaliaje na kama unaona unachoangalia.
Tunaweza kujiuliza hivi kwenye kazi pia.
Kwamba swali siyo unafanya kazi gani, bali unaifanyaje na kama unatoa thamani kubwa kwa wengine.
Rafiki, hakuna kazi au biashara fulani ambayo ukiifanya ndiyo utafanikiwa zaidi.
Kila kazi au biashara ina fursa kubwa ya mafanikio ndani yake.
Inategemea tu jinsi mtu anavyoifanya, kama amejitoa kuifanya kweli, kuifanya kwa ubora wa hali ya juu na kama anatoa thamani kubwa kwa wengine.
Dunia huwa inalipa thamani, kazana kuitoa na utalipwa.
Usihangaike na kujaribu kila aina ya kazi au biashara,
Chagua kile unachopenda au kujali, kifanye kwa ubora wa hali ya juu, toa thamani kubwa kwa wengine na mafanikio yatakuwa yako.
Usijiulize nifanye nini ili nifanikiwe zaidi, bali jiulize nifanyeje kile ninachofanya ili kufanikiwa zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania