“Almost everything will work again if you unplug it for a few minutes, including you.” – Anne Lamott
Kama umewahi kutumia kifaa chochote cha kielektroniki, iwe ni simu, tv, kompyuta, redio n.k, unajua pale kifaa hicho kinapokusumbua, hatua ya kwanza ni kukizima na kuwasha. Yaani ku RESTART.
Kabla hujakipekela kifaa hicho kwa fundi, unazima na kuwasha kwanza na mara nyingi kinakaa sawa, bila hata ya kukipeleka kwa fundi.
Hivi pia ndivyo mwili wako ulivyo,
Kuna wakati utajisikia kila dalili ya kuumwa, utajimbia kabisa hii ni malaria au ugonjwa mwingine uliozoea. Unaenda hospitali na kupima kila kitu na unambiwa huna ugonjwa.
Ulichokuwa unahitaji kwenye hali kama hiyo ni ku RESTART mwili wako, kuuzima halafu kuuwasha, kwa kujipa muda wakutosha wa kupumzika.
Kupumzika ni moja ya tiba muhimu sana unazoweza kuupatia mwili wako,
Hivyo kabla hujakimbilia hospitali au kupima pale ambapp hujisikii vizuri, hebu pumzika kwanza, utashangaa mwili unarudi vizuri na kuweza kuendelea na mambo yako.
Kuzima na kuwasha, kunasaidia vitu vingi, ikiwepo mwili wako, hivyo tumia njia hii kila mara kabla hujaingia gharama kubwa na kupoteza muda zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania