“War in this world can be stopped not by the ruling establishment, but by those who suffer from the war. They will do the most natural thing: stop obeying orders.” – Leo Tolstoy

Pale ambapo kuna mambo yasiyo mazuri yanayoendelea, anayeweza kutokomeza siyo yule anayefanya mambo hayo, bali yule anayefanyiwa na kuumia kwa mambo hayo.
Kama kuna vita, anayeweza kusimamisha vita hivyo siyo viongozi wanaoviendesha, bali wananchi wanaoumia na wanajeshi wanaopigana. Hawa wakikataa kutii maagizo yanayotolewa, hakuna vita.

Kama kuna ukandamizaji unaoendelea, atakayeutokomeza siyo anayekandamiza, bali anayekandamizwa, kwa kukataa kutii maagizo ya ukandamizaji anayopewa.
Upo usemi kwamba mtu mmoja ni mkandamizaji kwa wengi siyo kwa sababu ana nguvu sana, bali kwa sababu hao wengi wamekubaliana na ukandamizaji.

Chochote ambacho wengine wanakifanya kwako na hukubaliani nacho au hakina manufaa kwako, wewe ndiye mwenye nguvu ya kukitokomeza.
Usifikirie wale wanaofanya kuna wakati wataona siyo sahihi na waache, wao wataendelea kufanya kadiri utakavyoendelea kupokea.

Kataa kupokea na kutii maagizo ya chochote ambacho siyo sahihi kwako, ambacho kinakuumiza na hapo utaweza kukitokomeza.
Haitakuwa rahisi, lakini ukishaonesha msimamo wako na kutokutetereka, watu wataufuata.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kutokomeza yale ambayo siyo sahihi na watu wanayafanya kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania