“Nature created us related to each other, from the same material, for the same purpose. Because of this, somewhere within all of us is mutual love for each other.” —LUCIUS ANNAEUS SENECA

Sisi sote ni kitu kimoja,
Tuna umoja na viumbe wote waliopo duniani.
Wote tunategemeana ili maisha yaweze kwenda hapa duniani.
Hivyo ushirikiano mzuri ni muhimu kwa kila kiumbe ili kuweza kuwa na maisha bora.

Ili maisha yako yawe bora, kazana kufanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi.
Ili kuwasaidia wengine, anza kujisaidia wewe mwenyewe kwanza.
Huu ni msingi muhimu mno wa ushirikiano, wa kuwa na kitu cha kutoa na kupokea,
Badala ya kuwa ushirikiano wa upande mmoja tu, iwe kupokea tu au kutoa tu.

Uwe na siku bora ya leo, siku ya kushirikiana na wengine kwa sababu wote ni kitu kimoja.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania