Mara kwa mara, acha kile unachofanya na jiulize ni nini hasa unachotaka kwenye hicho unachofanya.

Ni rahisi sana kujisahau na kutoka nje ya mstari kama huna kitu cha kujipima mara kwa mara.

Lakini unapoacha na kujiuliza, ni rahisi kujikamata pale unapokuwa umetoka nje ya mstari wa kile ulichokuwa umepanga kufanya.

Unapojiuliza nini hasa unataka kwenye kile unachofanya, unapata mwanga wa wapi unataka kufika na iwapo unachofanya kitakufikisha kule unakotaka kufika.

Kupanga ni rahisi, lakini kutekeleza kile ambacho umepanga, ni kazi ngumu, kuna sababu nyingi sana zinazoweza kujitokeza na kukuondoa kwenye mpango wako.

Kuanza kufanya ulichopanga kunawezekana, lakini kutekeleza kwa viwango ambavyo ulikuwa umepanga siyo rahisi, katikati ya kufanya unaweza kunyemelewa na vitu vingine ambavyo vinaathiri ukamilishaji wako.

Hivyo kuwa na muda wa kujiuliza nini hasa unachotaka, ni njia nzuri ya kuhakikisha unafanya ulichopanga na unafanya kwa viwango vizuri.

Hufanyi tu ili kukamilisha, bali unafanya ili kupata matokeo unayoyategemea.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha