Never postpone a good deed which you can do now, because death does not choose whether you have or haven’t done the things you should have done. Death waits for nobody and nothing. It has neither enemies, nor friends. — INDIAN WISDOM
Kama kuna jambo zuri unapanga kulifanya leo, lifanye kama ulivyopanga.
Usiahirishe chochote kwa ajili ya kesho, kwa sababu huna uhakika kama hiyo kesho utakuwepo.
Kifo hakiangalii nani yiko tayari na nani hayuko tayari, kinamtembelea yeyote na wakati wowote.
Hivyo mara zote kuwa tayari, kwa kuhakikisha yale muhimu umeyafanya kama ulivyopanga bila kuahirisha.
Umepanga kufanya nini leo?
Nenda kafanye kama ulivyopanga na usiruhusu hali ya kuahirisha iwe kikwazo kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania