“A man who follows his wishes changes his attitude with time. Very soon he is not satisfied any more with the things he does.” – Leo Tolstoy
Usiwe mtu wa kuendeshwa na matakwa yako,
Badala yake ishi kwa misingi uliyojiwekea.
Matakwa hubadilika kila wakati,
Lakini misingi ni imara na ina msimamo.
Ili kufanikiwa, ni lazima uwe na misingi unayoiishi na kuisimamia wakati wote.
Ukiwa mtu wa kufuata matakwa yako, hutafanya lolote kubwa.
Kwa sababu unapofikia ugumu, matakwa yatakushawishi uache na kwenda kufanya kitu kingine.
Muda huu utatamani hiki, muda mwingine utatamani kingine.
Ukiona watu wana kitu fulani na wewe unakitaka.
Ni lazima uwe tayari kuukatalia mwili wako, kujiambia hapana kwa mambo mazuri sasa, ili upate mambo bora baadaye.
Usijidanganye kufuata matakwa yako kutakupa furaha, mwisho wa siku kutakufanya ujione wa hovyo na usiyefaa.
Maana ukifuata takwa moja, linakuja jingine na jingine na jingine.
Mwisho unajikuta umehangaika na mambo mengi, lakini hakuna matokeo bora uliyozalisha.
Kuwa na msimamo, ishi kwa misingi na siyo matakwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania