All that we know, we know through the intellect. Those who do not believe, people who say that you should not follow your intellect, remind me of those who suggest that you turn down the only lantern which shows you the way into the darkness. – Leo Tolstoy

Taa inayokumulikia gizani ni akili yako,
Hii ndiyo inayokuwezesha kujua kile unachopaswa kujua,
Hii ndiyo inayokupa jawabu la kila ugumu au changamoto unayokutana nayo.
Akili yako ina uwezo mkubwa sana.
Ipe jukumu lolote na italitekeleza,
Iambie unachotaka na itakuonesha namna ya kukipata.
Lakini hii yote ni kama utaweza kuitumia akili yako vizuri.

Wale wanaotaka kukutumia au kunufaika na wewe,
Wale wanaotaka uendelee kuwa mtumwa wao,
Wale wanaotaka kukuibia au kukutapeli,
Kitu cha kwanza wanachofanya ni kuhakikisha wanakuzuia usitumie akili yako.
Wanafanya kila namna ili usitumie akili, na ukishaacha kutumia akili, unapotea.
Kutokutumia akili yako kwenye kufanya maamuzi ni sawa na kuzima taa pekee inayokuongoza gizani.

Linda sana akili yako na itumie kila wakati, hhaitakuangusha.
Lakini usipoitumia, kila kitu kitakwenda vibaya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa, Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania