Ugonjwa wa mafua makali unaosababishwa na vizuri vya Corona unaoendelea kwa sasa duniani, siyo mwisho wa dunia.
Licha ya nchi nyingi kufunga kabisa shughuli zote za mikusanyiko na kuzuia safari za kuingia au kutoka kwenye nchi hizo, siyo mwisho wa dunia.
Dunia imewahi kupitia hali za hatari kuliko hii tunayopitia sasa, lakini binadamu tulishinda na maisha yakaendelea, kwa kuwa bora zaidi.

Hofu kubwa kwenye ugonjwa huu wa Corona ni uharaka na urahisi wa usambazaji wake.
Lakini kwenye madhara, hasa ya kifo, haujafikia magonjwa ambayo yamewahi kuitikisa kweli dunia.
Una uwezekano mkubwa wa kugonjwa na gari ukafa kuliko kupata Corona ukafa.
Kama una afya bora hata ukiupata ugonjwa huu, utapona na maisha yataendelea.
Katika watu 100 wanaougua ugonjwa huu, ni watu 2 mpaka 3 wanaokufa, na wengi ni wazee, wenye upungufu wa kinga na wenye magonjwa sugu.

Hivyo kuwa mtulivu na endelea na maisha yako,
Hatari siyo kubwa kama inavyochochewa na vyombo vya habari.
Usitaharuki, kuwa tulivu, fanya kile kilicho sahihi.
Huu ndiyo wakati sahihi wa kupima ukomavu wako kwenye Falsafa ya Ustoa, kama mafua haya yanakupa hofu, kama kila dakika unataka ujue nini kinaendelea, kama kuna mgonjwa mpya nchini, bado hujawa Mstoa na falsafa hii haihakusaidia.

Katika kipindi kama hiki, falsafa ya ustoa inamsaada katika kutupa utulivu,
Tunaangalia nini kipo ndani ya uwezo wetu na kukifanya,
Kisha kile kilicho nje ya uwezo wetu haturuhusu kitusumbue.
Tunajua kabisa kwamba hatutaishi milele, hivyo hata kama utakuwa mmoja kati ya wale watatu wanaokufa wakiugua ugonjwa huu, huna cha kuhofia, badala yake unapaswa kuishi vizuri leo, kutokuahirisha chochote kwa ajili ya kesho, kwa sababu hakuna mwenye uhakika wa kesho.

Kuhofia kwamba utakufa kwa Corona ni kichekesho, kwa sababu hata kama hutakufa kwa Corona, bado utakufa tu.
Na ukijiambia Corona itakuua kabla ya muda wako, unachekesha zaidi, nani alikuambia muda wako ni lini?

Tukirudi kwenye msingi wa ustoa, tunapaswa kilocho sahihi, kilicho ndani ya uwezo wetu.
Na kwenye mlipuko huu wa Corona unaoendelea, kuna mambo matano sahihi na yaliyo ndani ya uwezo wako kufanya;
1. Nawa mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara.
2. Usishikane au kugusana na mtu mwingine.
3. Usishike mdomo, pua au macho yako kea mikono ambayo hujaisafisha.
4. Epuka mikusanyiko isiyo na ulazima.
5. Acha kufuatilia vyombo vya habari kuhusu ugonjwa huu, hakuna kipya utakachojifunza zaidi ya kujazwa hofu.
Zingatia haya na utakuwa na utulivu mkubwa katika kipindi hiki ambacho dunia nzima imataharuki.
Na kama ndiyo kitu pekee ambacho kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA imekusaidia, basi ni hatua kubwa maishani mwako.

Uwe na wakati mwema, uwe tulivu, ishi kwa misingi ya Falsafa ya Ustoa.
Tumia vizuri kila ulichonacho leo, kwa sababu huna uhakika kama kesho kitakuwepo au wewe utakuwepo.
Usiipe hofu nafasi.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania